Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Latest Posts

Our Campaigns

  1. Adopt Child
    Campaign has ended
  2. Medical Treatment
    Campaign has ended
  3. Donate Clothes
    Campaign has ended
  4. Shelters For Needy
    Campaign has ended
  5. Hygienic Food
    Campaign has ended

Kuwa Kanisa la Mahali Pamoja Linaloamuru Matokeo Kwenye Mji

Waefeso 3:10 ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho;

Mungu akitaka kufanya jambo lolote hapa duniani kuna wakala wake, na hicho kituo kinaitwa Kanisa. Kanisa ni chombo cha Mungu cha kueneza hekima hapa duniani.

Kuna uelewa kuhusu kanisa ambao ni muhimu kufahamika na kila mwamini, kuna kanisa la ulimwengu wote ambalo hujumuisha watu waliomwamini Bwana Yesu waliopita, waliomwamini Bwana Yesu waliopo na watakaokuja;

Kanisa la mahali pamoja ni watu waliomwamini Bwana Yesu ambao lipo eneo moja la Kijiografia na lina uwezo wa kukutana katika eneo moja.

Hakuna siku kanisa la ulimwengu litakutana kwa mara moja; Kanisa la mahala pamoja, ndilo tafsiri ya kanisa la ulimwengu yaani kanisa la mahala pamoja ni udhihirisho wa kanisa la ulimwengu; namna kanisa la ulimwengu tunaliona, ni kwa kupitia kanisa kuliangalia kanisa la mahali pamoja.

Kanisa la mahala pamoja ni utekelezaji wa siku kwa siku wa kanisa la ulimwengu. Kuna vitu kanisa la ulimwengu limeaminiwa livitoe lakini utekelezaji wake unatokezwa katika kanisa la mahala pamoja.

Kanisa la mwanzo lilikua na mashtaka makubwa mawili:

  1. Kuupindua ulimwengu

Matendo 17:6 na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako,

  • Kuijaza miji na Mafundisho

Matendo 5:28akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.

VIFAA AMBAVYO KANISA LA KWANZA LILITUMIA KUUPINDUA ULIMWENGU;

  1. Kanisa lilikua na mikazo ya Kiroho

Kanisa ambalo litaamuru matokeo kwenye mji wowote, ni kanisa ambalo halijadili mikazo ya kiroho, mikazo ya kiroho ni ya kutekelezwa siku kwa siku.

Matendo 6:3-4 Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili; na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno.

Uelewa wa kanisa la mwanzo, ni kuwa ndani ya kanisa hakuna kazi au mtendakazi ambaye hastahili vigezo vya kiroho; vigezo vya kanisa la mwanzo ili ugawe chakula, upange viti, uwe mlinzi lazima uwe umejaa Roho; moja ya vitu ambavyo hatupaswi kushusha viwango ni vitu vya kiroho.

Mikazo ya kiroho; MKAZO WA MAOMBI

Kanisa la mwanzo lilikua linaomba kama mwitikio wa asili kwenye jambo lolote, ukiwafunga wanaomba, ukiwatisha wanaomba, ukiwapiga wanaomba; hawakua na mbadala wowote wa kuomba.

Kwa kadili watu wanakuwa na mbadala wa mikakati mingi ya utendaji, ndivyo ambavyo wanacha kuomba, na kadili wanavyoacha kuomba ndivyo wanakosa

  • Ukuaji endelevu kuyaelekea mambo ya Kiungu

MIFANO YA KUJIFUNZIA

Mfano #1: Stephano

Matendo 6:5,8-10 Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia; Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu. Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano; lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye.

Stephano alichaguliwa kama mgawa chakula; lakini alikua amejawa na Roho, amejawa na imani na amejawa, hekima na amejawa neno la Mungu kiasi kwamba masinagogi yalishindana naye na hayakuweza kushinda hekima, maarifa, na Roho aliyekua naye.

Mfano #2: Filipo

Matendo 8:6-8 Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa. Ikawa furaha kubwa katika mji ule.

Ili kanisa lilete mgeuko kwenye mjia, lazima kanisa lihakikishe kila mtendakazi anakua kiuendelevu katika mambo ya Kiungu.

Matendo 21:8-9 Asubuhi yake tukaondoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, mhubiri wa Injili, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake. Mtu huyu alikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiri.

Kanisa litaamuru matokeo katika mji lililopo lazima liwe lina mpango wa kuwaendeleza watu kuwa na uwezo wa kutendakazi za kiroho wenyewe bila kutegemea wachungaji.

Lazima kanisa liwe na mpango la kuendeleza watu baada yao; Sio tu Filipo aliokua mhubiri wa injili lakini aliweza kuzaa watoto wake na kuwainua kuwa watabiri.

  • Kanisa lililofundishwa kujidhabihu

Imani tuliyo nayo ni imani ya msalaba, ni imani ya mauti, ni imani ya damu; wakati wa Bwana Yesu msalaba ulikua ni jambo la hovyo sana tofauti na sasa

Kanisa liliamuru matokeo pale lilipofikia hatua ya kudhabihu maisha yao hata kufa. Kanisa walikua tayari kufa kwa sababu ya ujumbe walio ubeba.

Watu wanaojipenda sana kiasi kwamba wanajihurumia kiasi cha kufa huwa wanakufa

Dhabihu ni kusalimisha mambo ambayo ni haki na stahiki yako; kama vile ambavyo mtu ana haki ya kulala na akaamu kusalimisha muda wake wa kulala kwa ajili ya kazi anakua ametoa dhabihu. Kanisa ambalo haliamuru matokeo ni kanisa ambali limejaa watu wanaojihurumia na kutafuta mambo yao.

Ufunuo 2:10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.

Mathayo 16:24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.

  • Kutambua na kuheshimu neema zinazotenda kazi katika kanisa la mahala pamoja

Matendo 13:1-3 Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*